Chorus
Ombi moja twalileta kwako ee Maria (mama yetu)
Tujalie kufika mbinguni uliko mama
Tufurahi na watakatifu milele yote
Verse 2
Safari ni ndefu na magumu ni mengi
Mama tupe neema ya kufaulu
Verse 3
Dhambi zetu nyingi zinatusonga sana
Tujalie neema ya kuokoka
Verse 4
Hila za shetani na majaribu yake
Zatukinga njia kufika kwako
Verse 5
Pia twaombea na wasiokujua
Uwasaidie kufika kwako