SectionsExitNyota ya Matumaini

Nyota ya Matumaini

MarianExit
Verse 1

Mama yetu Maria, ni mama wa neema, tena ni kimbilio la watu wote wakosefu, ni msaada wa kweli mama tuombee

Chorus

Ni Nyota, ni Nyota, mama yetu Maria ni Nyota ya matumaini x2

Verse 3

Mlango wa mbinguni, sanduku la agano, malkia wa amani, malkia mwenye huruma, mama mpendelevu mama tuombee

Verse 4

Nyota ya asubuhi, ni mnara wa pembe, kimbilio la wakosefu mama utuombee, mama yetu Maria kiongozi wetu

Verse 5

Twakushukuru mama kwa maombezi yako, na kwa neema zote unazo tuombea mama, malkia wa amani mama tuombee