Verse 1
(Bara na bahari furahini sana
Tumemulikwa na nuru ya Mbinguni) x2
Chorus
Tumemulikwa na nyota ya bahari
Bikira daima (mulika) mulika nyoyo zetu
Tumeona leo mwangaza wa kweli
Somo wa kanisa (mulika) mulika njia zetun{(Mama) Mama tuombee, mamantuongoze, Kwa mwanao Yesu, kulenuwinguni } x2
Verse 3
Pendo lako mama, limetuvutia
Tunatangaza sifa zako kwa nyimbo
Bara shangilia, bahari ivume
Tumsifu mama, mama wa Maulanan
Piga tarumbeta, pigeni mluzi
Imbeni wimbo wa mama wa Mulungu
Chezeni pamoja, ruka juu juu
Mama wa Yesu afurahi Mbingunin
Mama wa Mwokozi, Malkia wa Mbingu
Mwanga angavu somo wa kwaya yetu
Uliyekingiwa dhambi ya asili
Daraja letu tuendao Mbingunin
Nyota za angani zamulika nchi
Mama Maria anamulika nyoyo
Usiku mchana anatuangaza
Tunatembea na nuru siku zote