Chorus
{ Nyanyukeni waumini wote tufanye shangwe
Kwa nderemo, kwa vigelegele na kwa vifijo } *2
Bwana asifiwe (sana) Bwana asifiwe (kweli)
Bwana asifiwe Mwathani aragoshuo
Verse 2
Nikiziangalia mbingu ni kazi ya vidole vyake
Mwezi na nyota za mbinguni ulizoratibisha wewe
Verse 3
Uwezo wake Bwana Mungu haupimiki kwa mizani
Mipango yake kwetu sisi haiwezi kubadilishwa
Verse 4
Alikausha baharí ya Shamu ikawa nchi kavu
Waisraeli wakapita kwa uwezo wa Mungu Baba
Verse 5
Na tupigeni tarumbeta vinubi hata na matari
Tuimbe wimbo wake Musa na ule wa Mwanakondoo
Verse 6
Pazeni sauti zenu kwa shangwe hata na vifijo
Sifa pia na utukufu tumpe Bwana siku zote