Chorus
(Nyanyukeni waumini wote tufanye shangwe
Kwa nderemo, kwa vigelegele na kwa vifijo ) *2
Bwana asifiwe (sana) Bwana asifiwe (kweli)
Bwana asifiwe Mwathani aragoshuo
Verse 2
Nikiziangalia mbingu ni kazi ya vidole vyake,
Mwezi na nyota za mbinguni ulizoratibisha wewe.
Verse 3
Uwezo wake Bwana Mungu haupimiki kwa mizani,
Mipango yake kwetu sisi haiwezi kubadilishwa.
Verse 4
Alikausha baharí ya Shamu ikawa nchi kavu,
Waisraeli wakapita kwa uwezo wa Mungu Baba.
Verse 5
Na tupigeni tarumbeta vinubi hata na matari,
Tuimbe wimbo wake Musa na ule wa Mwanakondoo.
Verse 6
Pazeni sauti zenu kwa shangwe hata na vifijo,
Sifa pia na utukufu tumpe Bwana siku zote.