Verse 1
Njooni wapenzi tufanye shangwe
Mwokozi Bwana amefufuka
Viumbe vyote tufanye shangwe
Mwokozi Bwana amefufuka
Chorus
Na tufanye shangwe, tuimbe aleluya
Mwokozi Bwana amefufuka
Verse 3
Leo mapema amefufuka -
Kaburi lake ameliacha -
Verse 4
Walinzi wake walishtuka -
Wakawa kama wamezimia -
Verse 5
Kwa ufufuko wako ee Bwana -
Umeturudishia uzima -
Verse 6
Umewashinda adui zetu -
Mauti kali pia shetani -
Verse 7
Enzi ni yako ya umilele -
Shukrani sifa na utukufu -
Verse 8
Hii ndiyo siku iliyofanywa -
Na Mungu nayo ni ya furaha -