Njooni tumwimbie Bwana wetu - kwa shangwe
Njooni kwa masifu kwa nderemo - tuchezen{Njooni tuabudu, njooni tusujudu
Tupige makofi,
Mbele zake Bwana, Mungu wa ulimwengu } *2
Hekalu lake Bwana Mungu linapendeza,
Nyumbani mwake Bwana mna mengi mazuri
Ninatamani kuingia nyumbani mwake
Nikae naye siku zote nyuani mwake
Nipate heri, mbele za Bwana
Mapema leo ninabisha lango ee Bwana
Nifungulie nipokee nipe faraja
Nimelemewa na mizigo mingi ya dhambi
Nyumbani mwake Bwana ndiko kuna uzima
Uzima tele, na usalama
Twendeni sote kwake Bwana Mungu Mwenyezi
Twendeni kwake tupeleke maombi yetu
Tutoe shukrani zetu kwa Mungu Baba
Tutoe na dhabihu zetu kwake Muumba
Sadaka zetu, azipokee
Uhai wetu unatoka kwake Muumba
Tuimbe sifa zake Mungu siku kwa siku
Tuyatangaze maajabu yake popote
Tuseme Bwana ametenda mambo makuu
Kwa watu wote, milele yote.