Chorus
{ Njooni njooni wote tumshukuru Mungu
Kwa mema mema mengi alotujalia } *2n{Ni mengi - ni mema mengi, haya-hesabiki kamwe
Tumepewa sote kwa ma-penzi yake yeye
Tumlipe nini Bwana ili naye apendezwe nasi
Kwa mema mema mengi alotujalia} *2
Verse 2
Ametuumba akili ya kutambua mema na mabaya
Ametujaza neema tumtambue,
Tuishi naye daima milele
Verse 3
Wengine katujalia uwezo na mali tumtumikie
Na wengine vipaji mbalimbali,
Ili tutambue uwezo wake.