Chorus
Njooni tuimbe, njooni tucheze, njoonintufurahi mbele zake Bwana. Piga makofi,npiga vigelegele shangilieni Bwana leo asubuhi
Verse 2
Sauti ya kwanza semeni alelluya
Sauti ya pili tumsifu Yesu Kristu.
Sauti ya tatu na ile ya nnenwaseme pamoja milele amina
Verse 3
Wa mama wote pigeni vigelegele
Wababa wote vinanda vipigwe sana.
Pigeni filimbi, ngoma na kayamba.
Watoto wadogo wachangamkeni
Verse 4
Mataifa yote njooni mbele za Bwana.
Makabila yote simameni tuimbe.
Nyanyukeni nyote pigeni makof,nshangwe, nderemo, vifjo machezo
Verse 5
Bahari na vitu vyote vivijazavyo.
Milima, mito na miti shangilieni.
Ndege wa angani na warukeruke,nwanyama kondeni furahini sana.