Njoo Moyoni

Baptism,Ordinary TimeEucharist
Verse 1

Njoo moyoni mwangu Bwana *2

Unishibishe mwili wako –

Unishibishe kwa mwili wako Bwana Yesu

Chorus

Ulisema alaye mwili wako

Ana uzima (iye iye) wa milele

Ulisema anywaye damu yako

Ana uzima (iye iye) wa milele

Verse 3

Njoo moyoni mwangu Bwana *2

Niburudishe kwa damuyo –

Niburudishe kwa damu yako Bwana Yesu

Verse 4

Mimi ni mdhambi ee *2

Unisafishe kwa damuyo –

Unisafishe kwa damu yako Bwana Yesu

Verse 5

Kaa ndani yangu ee Bwana *2

Na mimi nikae ndani yako –

Na mimi nikae ndani yako Bwana Yesu