Njia Za Mkato
Haraka hara-ka haina baraka,n(ndugu yangu) ka-wia ufike uendapo salama
Jifunze subi-ra na uvumilivu,n(fanya kazi) usipende kupata vya rahisi vya bure
Haupendi kuchoka - wala kutoa jasho
Wategemea - mali ya ndugu yako
Haupendi kungoja - wala kuulizia
Unafuata - njia za vichochoro!n
Njia za mkato ee -
Njia za mkato ee ni hatari sana
Zenye mabonde na maporomoko ee-
Na maporomoko ee ni hatari sana
Hizo za vichochoro ee-
Za vichochoroni ee ni hatari sana
Humo wamejaa na wanyang'anyi ee-
Nao wanyang'anyi ee ni hatari sana jihadhari sana
Mbona unataka mali upesi pasipo kutoa jasho
Vijia vya mkato unavipenda
Unaiba wala rushwa unavuna usikopanda
Majibu ya haraka unayapenda
Mbona unafurahia uzinzi pasipo kufunga ndoa
Vijia vya mkato unavipenda
Unapolemewa na ndoa wamkimbilia mganga
Majibu ya haraka unayapenda
Mbona unapokosea wewe wajitetea kwa uongo
Vijia vya mkato unavipenda
Unapokosana na ndugu wasuluhisha kwa vita
Majibu ya haraka unayapenda