SectionsEucharistNjia Ya Msalaba

Njia Ya Msalaba

LentEucharist
Verse 1

Umekosa nini we Yesu

Kushitakiwa bure kwa pilato

Mwenye kustahili hukumun(Si wewe si wewe Bwana ni sisi) x2

Verse 2

Ole msalaba huo mzito

Apagazwa mwana mpenzi wa Mungu

Mwili waenea mateson(Alipa alipa madhambi yetu) x2

Verse 3

Ona Muumba mbingu na nchi

Yupo chini mzigo wamwelemea

Na mtu kiumbe chake kwa ukalin(Ampiga ampiga bila huruma) x2

Verse 4

Huko njiani we Maria

Waonaje hali ya Mwanao

Ni damu tupu na vidondan(Machozi machozi yamfumba macho) x2

Verse 5

Kwa Simon heri ya kweli

Mimi pia Yesu nisaidie

Kuchukua mzigo wa ukombozin(Kuteswa kuteswa pamoja nawe) x2

Verse 6

Uso wa Yesu malaika

Bethlehemu walikuabudu

Bahati yake Veronican(Kupangusa kupangusa Mfalme wanmbingu) x2

Verse 7

Wakimvuta huku na huku

Wauaji wanamchokesha bure

Chini wamtupa bado kwa nguvun(Aibu aibu yao milele) x2

Verse 8

Wanawake waisraeli

Musilie kwa sababu hiyo

Muwalilie hao kwa dhambin(Upanga upanga ni juu yao) x2

Verse 9

Mwokozi sasa ni ya tatu

Waanguka chini ya msalaba

Katika dhambi za ulegevun(Nijue nijue kutubu hima) x2

Verse 10

Muje malaika wa mbingu

Funikeni mwiliwe kwa huruma

Vidonda vyake na utupun(Askari askari wamemvua) x2

Verse 11

Hapo mkristu ushike moyo

Bwana wako alazwa msalabani

Mara miguu na mikonon(Yafungwa yafungwa kwa misumari) x2

Verse 12

Yesu mpenzi nakuabudu

Msalabani unapohangaika

Nchi yatetemeka kwa hofun(Najua najua linaffa) x2

Mama Maria mtakatifu

Verse 13

Upokee maiti ya mwano

Tumemuua kwa dhambi zetun(Twatubu twatubu kwake na kwako) x2

Verse 14

Pamoja nawe kaburini

Zika dhambi na ubaya wa moyo

Yesu tuwe Wakristu kwelin(Twakupa, twakupa sasa mapendo) x2

Verse 15

Katika Roho yangu, Bwana

Chora mateso niliyokutesa

Nisiyasahau madenin(Na kazi na kazi ya kuokoka) x2