Nitumwe Mimi

Lent,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Lent,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary TimeThanksgiving
Verse 1

Hayo mliyofunuliwa, bila kuyalipia kitu, (nayo) ndiyo,

Yale mliyotumwa, kwenda kwa walio wadogo

Mungu alowatunukia awe mkuu pekee yaken(Jiulize) nani kwenu (aliyeomba) kuzaliwa!n(Jiulize tena) nani kwenu (anaijua) siku ya kufa!

Hakuna! Hakuna! ha!

Chorus

Hakuna jambo mnalomiliki hapa duniani

Yote mliyo nayo yana mwenyewe mnamjua

Naye amewapa haya kusudi mtumikiane

Ili kusiwepo na matabaka miongoni mwenu

Hiyo ndiyo hekima - ee aa een[b:] Hiyo ni hekima ni hekima tele

Hiyo ndiyo hekima -ee aa ee

Ndugu hiyo ndiyo hekima ya kweli

Verse 3

Kama mliyo nayo yote yangekuwa yenu

Hiyo pumzi mnayojivunia wapendwa,

Isingekuwa inakiogopa kichomi

Ingeendele-a hata palipo kichomi!

Verse 4

Uzuri wa sura zenu zenye ngozi laini

Inakuwaje hamuwezi kuelekeza,

Usiungue hata kwenye maji ya moto

Na usioze unapolala kaburini!

Verse 5

Elimu na vyeo vyenu na mamlaka yenu

Akili nyingi ufundi navyo vipaji vyenu,

Mbona hamvitumii mkiwa usingizini

Na mnaota ndoto sawa na za watoto!

Verse 6

Basi mimi, ninahimizwa, kujiepusha, kujiinua

Nijishushe mbele ya wote, wawe wakubwa au wadogo

Nisijiinue kati ya watu hata siku moja,

Badala yake nijinyenyekeze ili nifikike,

Akihitajika atakayewatumikia watu

Nijitokeze kwa haraka ili wanitume mimi, daima

Verse 7

Nijitokeze kusudi wanitume mimi

Nijitokeze, kuitikia wito daima

Nijitokeze kusudi wanitume mimi

Na nikitumwa niwe mwaminifu daima

Nijitokeze kusudi wanitume mimi

Nijitokeze wanitume na Mungu atukuzwe daima

Nijitokeze kusudi wanitume mimin

Verse 8

Nijitokeze, nijitokeze leo

Nijitokeze kusudi wanitume mimi

Nijitokeze, nijitokeze daima

Nijitokeze kusudi wanitumie mimi, milele!