Verse 1
Nitakwenda kwa shangwe na vigelegele
Niingie nyumbani mwa Bwana Mungu wetu
Chorus
Nitacheza, nitaruka, nitaimba wimbo ule mtamu
Baba njooni, mama njooni, tufurahi mbele za Mungu wetu
Verse 3
Njooni nyote wazee vijana na watoto
Mshangilieni leo nyumbani mwake Bwana
Verse 4
Nitatangaza sifa zake Mungu Mwenyezi
Kwenye kusanyiko nitakuimbia wewe
Verse 5
Nitasema asante kwake Mola Rabuka
Kwa ukarimu wako usio na kifani
Verse 6
Nitatoa shukrani zangu kwako Muumba
Nitakushukuru leo kesho na daima