SectionsThanksgivingNiseme Nini Ee Bwana

Niseme Nini Ee Bwana

Lent,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Lent,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary TimeThanksgiving
Chorus

Niseme nini ee Bwana, nitamke maneno gani kinywani

Nikushukuru jinsi gani,

Nisimulie vipi mimi, mapito niliyopita kuja hapa

Nikutukuze vipi Mungu

Niseme tu, Bwana Mungu wangu, asante nakushukuru

Narudia, Bwana Mungu wangu, asante nakushukuru

Verse 2

Nakumbuka nilivyojaribu, sikujua kama utajibu

Nikapapasa mkono kizani, kulipokucha ni tunda mkononi

Verse 3

Katikati ya safari maji yale yakamwagika chini

Lakini kwa wema wako, umeyazoa yakajaa upya

Verse 4

Nilipigwa mawe nikaaibishwa sana

Tazama leo umeniona, ukamtukuza mtumishi wako