SectionsEucharistNiruhusu Ee Yesu

Niruhusu Ee Yesu

Ordinary TimeEucharist
Chorus

Niruhusu Yesu wangu, niijongee meza yako

Unisamehe dhambi Mwokozi,nuje rohoni mwangu uniokoe

Njoo kaa ndani yangu, nami nikae ndani yako

Ili nipate amani tele, ndani ya Roho yangu nifarijikenn{ Wewe Bwana (wewe Bwana wanijua)

Wanijua (hata nafsini mwangu)

Wewe ndiwe tabibu pekee wa roho yangu

Tena ndiwe kimbilio langu }*2

Verse 2

Tazama Yesu wangu ninajongea karamu yako

Pengine kwako Bwana sikustahili kuijongea

Unihurumie ee Yesu wangu unisamehen

Hakika kwako Bwana makosa mengi nimeyatenda

Ubinadamu wangu siwezi kuficha kwako Bwana

Unihurumie ee Yesu wangu unisamehen

Niwazi Yesu wangu unaujua udhaifu wangu

Sina chakujitolea mbele yako Ee Yesu wangu

Unihurumie Ee Yesu wangu unisamehe