Verse 1
Ninataka kuingia, mjini mwa Mungu
Nitashinda nitakaza mwendo nifike
Nikishikwa na shida, nikichoka njiani
Yesu unaniambia uningojee
Verse 2
Naitwa na Yesu Kristu enzini mwake
Nakimbia kukawia hakuna faida
Wote wachelewao hawatapata taji
Mimi sitaki kingine ila uzima
Verse 3
Elekeza macho yangu mlangoni pako
Niongoze nipe nguvu nikilemewa
Ninapojaribiwa, ninaposingiziwa
Yesu unisaidie nisikuache
Verse 4
Mkono wako unishike nisianguke
Najiona kuwa mnyonge nguvu i kwako
Neno lako ee Yesu linanipa uzima
Nikifika nitaimba umeniponya