SectionsEntranceNinakulilia

Ninakulilia

LentEntrance
Verse 1

Ninakulilia Bwana Mungu, nipe neema zakonili shetani asinishinde, niwe wako milele *2

Verse 2

Uwe ndani yangu siku zote, Baba usiniache

Niwe ndani yako siku zote, niwe wako milele

Verse 3

Haki yako na idumu duniani siku zote

Uangaze roho yangu nikutii daima

Ee Baba unilinde

Verse 4

Ee Baba utazame, dunia yageuka

Ndugu wauana, magonjwa yamezidi

Verse 5

Upendo na haupo, kati ya majirani

Kwa kuwa haya yote, ni mwisho wa dunia

Verse 6

Ee ndugu tukumbuke (kwamba) raha za duniani (ovyo)

Kuna faida gani (kweli) kufuata ulimwengu

Na mwisho tusiishi na Baba Mungu ? *2