Verse 1
Ninakuabudu Mungu wangu
Unayejifcha altareni
Ninakutolea moyo wangu
Usiofahamu siri yakon
Mafahamu yangu yadanganya
Yanapokuona na kugusa
Namsadiki Yesu hadanganyi
Yeye Mungu Mwana na Ukwelin
Waficha umungu msalabani
Na ubinadamu altareni
Nami naungama yote mbili
Kama mwivi yule mwenye toban
Tomaso aligusa majeraha
Nami nasadiki bila shaka
Ewe Yesu nipe pendo lako
Tumaini kwako na imanin
Umeteswa nini Bwana mwema
Kwaku nipa mkate wauzima
Yesu unifiche ndani yako
Ili nilionje pendo lakon
Yesu pelikane nitazame
Na kwa damu yako nitakase
Tone moja ndilo linatosha
Na dunia yote yaokokan
Ndani ya mafumbo Yesu yumo
Atafumbuliwa kwangu lini
NikuoneYesu usowako
Nishiriki nawe heri yako AMINA.