Verse 1
Ninakuabudu Mungu wangu,
Unayejificha altareni,
Ninakutolea moyo wangu,
Usiofahamu siri yako.
Verse 2
Mafahamu yangu yadanganya,
Yanapokuona na kugusa,
Namsadiki Yesu hadanganyi,
Yeye Mungu Mwana na ukweli
Verse 3
Waficha Umungu msalabani,
Na ubinadamu altareni,
Nami naungama zote mbili,
Kama mwivi yule mwenye toba.
Verse 4
Thomas aligusa majeraha,
Nami nasadiki bila shaka
Ewe Yesu nipe pendo lako,
Tumaini kwako na imani
Verse 5
Umeteswa nini Bwana mwema,
Kwa kunipa mkate wa uzima
Yesu unifiche ndani yako,
Ili nilionje pendo lako
Verse 6
Yesu Pelikane nitazame,
Na kwa damu yako nitakase
Tone moja ndilo linatosha,
Na dunia yote yaokoka
Verse 7
Ndani ya mafumbo Yesu yumo,
Atafunguliwa kwangu lini?
Nikuone Yesu uso wako,
Nishiriki nawe heri yako. Amina.