Ninajiskia Mzuri
Ninajisikia mzuri (mimi) na mkamilifu
Ninajisikia mkweli (tena) nisiye na hila
Ninajisikia msafi (mimi) kwa matendo yangu
Ninajisikia ni mwema (tena) nisiye na dhambi
Mbele ya watu najituma, kama mtu mwema
Matendo yangu polepole, ya unyenyekevu
Kumbe huu ni wasifu wangu, wasifu wa nje
Wa ndani mwenendo mbaya wenye sifa mbaya
Kupenda mambo ya uwongo, tena ya uzushi
Daima nayasisitiza, ndiyo kazi yangu
Majirani wakigombana ninasikiliza,
Kumbe chanzo cha yote hayo, hii ni siri yangu
Ninakitumia kioo, ninajing'arisha
Kana kwamba mwuumba wangu alinikosea
Kumbe kwa nje napendeza, kama malaika
Kwa ndani mimi ni shetani, mwenye pembe kali
Hebu tazama moyo wako, ukaubadili
Kimatendo hata mawazo, uwe mtu mwema
Mwenendo mbaya daima unafananishwa
Na kumpepea shetani asichoke kwa kazi