SectionsThanksgivingNinaikumbuka Siku

Ninaikumbuka Siku

Lent,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary TimeThanksgiving
Chorus

Ninaikumbuka siku ile niliyokuita Bwana wangu

Ukaniponya na kuniepusha na hatari mbaya ya kifo

Mwili wangu uliopatwa na majeraha makubwa

Yenye maumivu makali na ya kutisha

Na ya kukatisha tamaann{n/b/

Nitamke maneno gani, niimbe wimbo gani mimi

Nicheze ala gani au niipige ngoma gani

Kama asante na shukrani yangu Bwana

Na nitoe sadaka gani, iwe kama shukrani yangu

Nikikumbuka wema wako, nisifuje Bwana wangu

Wewe ni mwenye huruma na upendonn/w/

Maneno gani mimi nitamke, na wimbo gani niimbe

Mimi nipige ngoma ganinkama asante na shukrani yangu Bwana

Sadaka nikutolee ee Bwana,nni kama shukrani yangu, nikusifuje Bwana wangu,

Wewe ni mwenye huruma na upendo } * 2

Verse 2

Ninakumbuka siku ile mimi niliposhindwa

Na maumivu ya majeraha ya kichwa niliyoyapata

Maumivu makali mimi yalinibana sana

Hata mwili ulikosa nguvu na fahamu kunipotean(Mimi ) mimi Bwana (niseme) niseme asante

Kukushukuru ee Mungu wangun(Mimi) mimi Bwana (nisipo) nisipotamka nitakuwa sina fadhila

Verse 3

Ninakumbuka siku ile mikono yangu mimi

Ilipopatwa na maumivu yaliyotokana na ajali

Mikono yangu mimi ilitokwa na damu nyingi

Hata na mifupa yangu iliyovunjika na kutokezan(Mimi ) mimi Bwana (niseme) niseme asante

Kukushukuru ee Mungu wangun(Mimi) mimi Bwana (nisipo) nisipotamka nitakuwa sina fadhila

Verse 4

Nilipopata fahamu nikajaribu kusimama

Mwili ulikosa nguvu kwa maumivu tena makali

Miguu yangu inatokwa damu nyingi na kunitisha

Hata na mifupa yangu iliyovunjika na kutokeza. . .n(Mimi ) mimi Bwana (niseme) niseme asante

Kukushukuru ee Mungu wangun(Mimi) mimi Bwana (nisipo) nisipotamka nitakuwa sina fadhila

Verse 5

Usingizi mzito ulinibeba na kunifanya

Niyasahau maumivu yangu yote niliyo nayo

Maumivu makali tena ya ndani yalinibana

Hata kuhema siwezi kugeuka hadi nisaidiwe . . .n(Mimi ) mimi Bwana (niseme) niseme asante

Kukushukuru ee Mungu wangun(Mimi) mimi Bwana (nisipo) nisipotamka nitakuwa sina fadhila

Verse 6

Hebu jiulize ndugu ni wangapi wanaopata haya

Hata uhai wao hutoweka na usirudi

Jitafakari ndugu wewe uzima uliojaliwa

Hata asante kwake Muumba tazama umemsahau, .n(Mimi ) mimi Bwana (niseme) niseme asante

Kukushukuru ee Mungu wangun(Mimi) mimi Bwana (nisipo) nisipotamka nitakuwa sina fadhila