SectionsExitNinafikiria Sana

Ninafikiria Sana

Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary TimeExit
Chorus

Ninafikiria sana na kutafakari jambo hili mimi

Jinsi ulimwengu ulivyogeukageuka kama kinyonga

Ukweli umegeuka na kufanyika kuwa uwongo leo

Msema kweli muovu muongo, yeye wakili wa mambo yoten

Shetani mbaya amezizunguka roho za watu

Anawadanganya kwa mambo mazuri pia na anasa,

Kanuni zake ngumu amri zakennazo zinashangaza shangaza

Mbuzi wa kijani, ng`ombe wa dhambarau

Kuku mwenye pembe, huyo utampata wapi

Njoo kwake Yesu (Mwokozi) hahitaji haya (yote)

Kanuni tubu dhambi, uingie mbinguni kwa baba

Verse 2

Anakudanganya atakupa fedha uwe ni tajiri

Kanuni zake yeye hudhulumu maskini na wajane

Amelaaniwa amelaaniwa afanyaye haya,

Kizazi chake yeye kitakuwa ni laana na fedheha

Maisha yake yeye ni nchi kame na yenye chumvi nyingi

Verse 3

Anakudanganya pombe inaweza kukuliwaza

Utafune mifupa ungali bado ukiwa na meno

Unafanya haya na watoto wako wanalala njaa,

Na wewe kijana wazazi nyumba inawangukia

Mwisho unapotea maisha yako wewe unachemsha

Verse 4

Sikieni sasa enyi mnaoufanya ukahaba

Mkijidanganya miili ni yenu sio ya yeyote

Nani anaweza kujiongeza hata unywele wake

Aliyekulea angefanya hivyo ungekuwa wapi

Na Mungu naye asingekuumba wewe ungekuwa wapi

Verse 5

Sikieni enyi mfanyao vita pia migogoro

Hamuoni kuwa hayo ni machukizo kwake Mwenyezi,

Mungu ameumba nchi nzuri yenye rutuba na mwanga

Na sisi binadamu twaharibu kwa mabomu na risasi

Tukumbuke ya kwamba mwisho tutalipa tutalipa haya

Verse 6

Jukumu ni letu sasa tuzitubu dhambi zetu zote

Tuliyoyafanya tumuombe Mola wetu asamehe,

Tutakuwa safi dunia yote itajaa amani,

Maisha yatakuwa ni rahisi utovu hamna tena,

Na wote tutakuwa jamii yenye maendeleo bora