Nimetunukiwa Tuzo
Thanksgiving
Chorus
(Nimetunukiwa tuzo lenye dhamani
Nimeletewa zawadi toka mbinguni
Nimejishindia mwana wa Mungu
Nimepewa Yesu zawadi tosha.) *2
Verse 2
Ninashangilia naimba kwa furaha
Ninarukaruka nacheza kwa furaha
Napiga makof ngoma na kayamba
Nimepata Yesu tuzo la ajabu (mimi
Verse 3
Ninakushukuru we Mungu Baba yetu
Nasema asante kwa mema yako yote
Napiga vinubi ngoma na kayamba
Nimejishindia Bwana wa mabwana (mimi)
Verse 4
Nikiwa na Yesu magonjwa yanapona
Nikiwa na Yesu mashaka yamekwisha
Yesu kiongozi Yesu jemedari
Yesu mchungaji Yesu mambo yote (mimi)
Verse 5
Maisha marefu ni tuzo nimetunzwa
Uzima milele nimeshaahidiwa
Mbinguni kwa Baba nitakaribishwa
Kwa maisha mema siku zangu zote (mimi)