SectionsThanksgivingNimetambua Makusudi Ya Bwana

Nimetambua Makusudi Ya Bwana

Ordinary Time,Ordinary TimeThanksgiving
Verse 1

Nimetambua makusudi ya Bwana

Kwa wale wote aliowapenda

Bwana huwafanya wapondeke moyo

Huwashusha mbele ya mataifa

Chorus

Bwana watambua nakupenda

Tegemeo langu liko kwako

Nia zangu zote ziko kwako

Bwana wajua ninapoketi

Pia wajua ninaposimama

Ninakukabidhi moyo wangu

Verse 3

Walio wake lazima kuteseka

Katika siku zote za maisha

Wajikane na waache ya dunia

Na wajivike misalaba yao

Verse 4

Machukizo ni lazima yatokeenlakini ole anayeyaleta

Moyo wa mteule hujaa furaha

Akiteswa kwa ajili ya Yesu

Verse 5

Nitayapokea kwa saburi kubwa

Mateso na machungu ya dunia

Ili nivikwe taji la utukufu

Nitakapofika mbele ya Yesu