SectionsExitNimemwacha Wapi Bwana

Nimemwacha Wapi Bwana

Lent,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary TimeExit
Verse 1

Mimi ni kitu gani na niko wapi, ninatoka wapi

Ninakwenda wapi, mimi nimemwacha Bwana wangu nimtumainiaye

Kaniumba kanitofautisha na wanyama kwa utashi

Ndiye anayeitegemeza nafsi yangu mchana usiku hunilinda

Chorus

{Nimemwacha wapi (Bwana) Bwana wangunmimi naenda kujiongoza

Imani yangu imekuwa nia tu siku hadi siku

Matendo yangu yamekuwa ni kinyume toka kitambo

Kwa ajili hii ona ninafanya kazinna kujinyima nafsi yangu mema } *2

Verse 3

Maisha yangu ni safari tangu kuumbwa kuzaliwa

Na kuishi kwangu hapa duniani mwisho nipate uzima wa milele

Yeye anipaye pumzi ya uhai wangu na mlinzi wa maisha yangu

Kwa kila hatua ya maisha yangu hapa duniani

Verse 4

Kanisani nakwenda natoa sadaka na zaka

Lakini ulevi mimi unanitawala kwani pombe ndiye wangu mfariji

Anasani maishani yake na ya famili yake

Na gizani uzinzi ni wangu rafiki sakramenti ya ndoa iko wapi

Verse 5

Watoto wapatao mali kwa mganga kupiga bao

Nyumba nayo izindikwe hirizi, mikononi nami urogi kaurithi

Kutosita hio nihoji ndugu na jirani

Ati jirani yule ndiye jina fulani nikimsema kusengenya napenda

Verse 6

Maana sheria zako ni kama kioo mbele ya matendo yangu,

Moyo wangu wanielemea nikitafakari matendo yako

Maana sheria zako ni kama kioo mbele ya imani yangu,

Maisha yangu yamekuwa gizani tena ni maisha ya dhambi

Verse 7

Ewe ndugu yangu jiulize moyo wako uko wapi

Na matendo yako yampendeza Muumba wako kwa uzima alokupa

Ewe Baba mama vijana ewe mlei hebu jiulize

Mwisho wa maisha yako haya utaupata uzima wa milele