SectionsThanksgivingNilikuomba Unipe

Nilikuomba Unipe

Wedding,Ordinary Time,Ordinary Time,Wedding,Ordinary Time,Christmas,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary TimeThanksgiving
Verse 1

Nilikuomba unipe (nipe) nguvu nipate kufanikiwa

Nawe ukanipa udhaifu nipate kumnyenyekea Mungu

Nilikuomba unipe (nipe) afya nitende mambo makubwa

Nawe ukanipa maradhi nitende mambo mema zaidi

Chorus

Asante Mungu (twakushukuru) kwa wema wako wote

Maana wewe u mwema, umenihurumia umenijalia mema yote

Umeninyima yote (mabaya) ukanijalia yote (haya)

Maana nayahitaji, umenihurumia umenijalia mema yotenn{Nasema ee Mungu - Na sasa ee Mungu wangu mpenzi

Na sasa ee Mungu - Napenda kukiri neno hili moja

Kati ya watu - Kati ya watu wa ulimwengu

Nimebarikiwa - nimebarikiwa mno ee Mungu asante} *2

Verse 3

Nilikuomba nipe utajiri nipate kujaa furaha

Nawe ukanipa ufukara nipate kuishi kwa busara

Nilikuomba nipe mamlaka wapate kunisifia

Nawe ukanipa udhaifu nipate kumhitaji Mungu

Verse 4

Nilikuomba nipe kila kitu nifurahie maisha

Nawe ukanipa uhai nivifaidi vitu vyote

Nilikuomba unipe na ujanja nionekane hodari

Nawe ukanifanya mjinga nijifunze kumtii Mungu

Verse 5

Nilikuomba nipe maarifa nipate kujulikana

Nawe ukanifanya mnyonge nipate kumtumaini Mungu

Nilikuomba unipe enzi nipate kumiliki nchi

Nawe ukanitia majonzi nipate kumkimbilia Mungu