SectionsOffertoryNikupe Nini Mungu Wangu

Nikupe Nini Mungu Wangu

Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Wedding,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Wedding,Marian,Ordinary Time,Ordinary Time,Resurrection,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Resurrection,Ordinary Time,Christmas,Wedding,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary TimeOffertory
Chorus

{ Nikupe nini Mungu wangu, nikupe nini we Mwokozi

Nikupe nini Bwana wangu cha kukupendeza } *2

Verse 2

Kila nitakachoshika mbona bado ni kidogo

Fadhili unazotenda kwangu mimi naogopa

Ninakuomba Mwokozi, nifanyie msamaha na unipokee

Mema unayoyatenda, nitafanya nini mimi nikurudishie

Verse 3

Nakutolea mkate toka mmea wa ngano

Nakutolea divai ni tunda la mzabibu

Ninakuomba Mwokozi . . .

Verse 4

Mchana hata siku wewe wanisimamia

Na nikiwa safarini waniepusha ajali

Ninakuomba Mwokozi . . .

Verse 5

Nikiwa na matatizo Bwana wanisaidia

Nikiwa kwenye majonzi Bwana unanifariji

Ninakuomba Mwokozi . . .

Verse 6

Kama njia siioni Bwana unaniongoza

Na hata nikipotea kwako unanirudisha

Nitatoa nini mimi, kitakachokuwa sawa, na fadhili zako

Nitaimba vipi mimi, niyataje mema yote, utendayo kwangu