Verse 1
Nikupe nini ee Mungu cha kukupendeza,nuwezo wangu mdogo Bwana waujuanpamoja na dhiki inayonisonga pokeanzawadi yangu hii duni
Verse 2
Nikitazama wenzangu, wanakutoleanzawadi nyingi na nzuri za kukupendeza,nkasoro mimi tu, natoa kidogo. Wakatinmwingine, sitoi kabisa
Verse 3
Maisha yangu ya dhiki Bwana wayajua
Unyonge na udhaifu wangu waujua
Sina kitu mimi, cha kukutolea, lakininpokea nafsi yangu Bwana
Verse 4
Nayakabidhi maisha yangu kwako
Bwana uniongoze katika njia ya uzimanunisaidie wakati wa shida, kwani ninwewe tu tumaini langu
Verse 5
Kutoa ndugu ni moyo siyo utajiri
Ukimtolea Mungu atakuongeza,nuwasaidie watu maskini wasiojiwezanutabarikiwa
Verse 6
Ninawasihi wenzangu mliojaliwa
Maisha bora mazuri naya kuridhisha
Msimsahau, Bwana Mungu wenu,
Toeni kwa wingi mtabarikiwa.