SectionsOffertoryNikulipe Nini

Nikulipe Nini

Ordinary Time,MarianOffertory
Verse 1

Nikulipe nini ewe Mungu Baba wa Mbinguni

Kwani mtu mimi sina kitu cha kujivunia

Chorus

Uhai na nguvu ni zawadi nzuri umenipa wewe Baba.

Maisha mazuri ni talanta safi nimepata kwako wewe

Sasa nakuomba baba nigeuze chombo chako

Nimejitolea kwenda kutangaza neno lako *2

Verse 3

Nikufananishe na nini humu ulimwenguni

Uliumba vyote bahari mito hata milima

Verse 4

Ningekuwa ndege hakika ningeruka angani

Ningekuwa nyota ningemulika dunia yote

Verse 5

Nitakutendea nini ili nikufurahishe,

Nitakuimbia wimbo gani Baba nikusifu

Verse 6

Unitume Baba popote nipeleke ujumbe

Nitalihubiri Jina lako daima milele