SectionsThanksgivingNikiziangalia Nchi

Nikiziangalia Nchi

Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Wedding,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Wedding,Marian,Ordinary Time,Ordinary Time,Resurrection,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Resurrection,Ordinary Time,Christmas,Wedding,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary TimeThanksgiving
Verse 1

Nimezitafakari habari za anga na maji

Nikainua macho yangu, kuitazama nchi kavu

Na miondoko ya viumbe wote waliomo

Sauti zao na tamaduni zao

Chorus

Nikiziangalia nchi na pande zake zote

Nikiitazama milima na mabonde yote

Utukufu wako nakupa Mungu wangu

Sifa na heshima

Utukufu wako nakupa Mungu wangu

Na enzi ni yako

Utukufu wako nakupa Mungu wangu

Daima milele

Utukufu wako nakupa Mungu wangu

Verse 3

Wanyama juu ya anga na ndege wote angani

Samaki nao baharini na mimea ya ardhini

Wote umetoa wewe uhai ukaanza

Dunia yote ikawa furaha

Verse 4

Ili kuondoa upweke ukaanzisha lugha

Viumbe tuwasiliane tupate kukamilishana

Upendo gani huu kwa tusioweza shukuru

Ingawa tunafurahia kupendwa

Verse 5

Unafahamu shida zetu na mahitaji yetu

Mipango yetu ya maisha daima unainyoosha

Ingawa macho yetu hayajawahi kukuona

Lakini daima hautusahau

Verse 6

Ningetamka moja moja sifa zako Mwenyezi

Lakini ni nyingi sana na akili yangu inaganda

Nabaki kutabasamu ninapokukumbuka

Halafu ninaimba wimbo wa shangwe