Chorus
Nifanye nini Mungu wangu
Ili nikae nyumbani kwako daima *4
Verse 2
Nainua moyo wangu kwako wewe Mungu wangu,
Unikinge na uiovu tumaini wewe tu
Verse 3
Nijulishe njia zako, nifundishe ukweli
Hekimayo niongoze, tumaini wewe tu.
Verse 4
Ewe Baba ukumbuke wema zako milele
Nifutie dhambi zangu, tumaini wewe tu
Verse 5
Nitazame kwa huruma ewe Mungu amini
Nitubishe mwenye dhambi tumaini wewe tu