Niacheni Mimi
Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Wedding,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Wedding,Marian,Ordinary Time,Ordinary Time,Resurrection,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Resurrection,Ordinary Time,Christmas,Wedding,Ordinary TimeEntrance
Verse 1
Niacheni mimi niimbe nimwimbie Muumba wangu
Niacheni mimi nicheze mbele zake Mwenye upendo
Chorus
Watu wote (leo) Nipisheni (mimi)
Nimwonyeshe Bwana Mungu wangu jinsi ninavyompenda
Nitaimba (mimi) nitacheza (sana)
Nitarukaruka kwa furaha nikimsifu Mwenyezi
Kwa nini nisiimbe(mimi), kwa nini nisicheze (mimi)
Nami ninapoimba ninasali mara mbili
Wanyama wanacheza wadudu wanarukaruka
Wanamsifu Mungu wao siku zote kwa furaha
Verse 3
Niacheni mimi niseme mbele zenu watu wa Mungu
Niacheni niyatamke yaliyonijaa moyoni
Verse 4
Niacheni niyaeleze maajabu ya Mungu wetu
Niacheni niyaeleze aliyonitendea Mungu
Verse 5
Niacheni niwaambie jinsi Bwana anipendavyo
Niacheni nisimulie leo kesho hata milele