SectionsEntranceNi Siku Kubwa

Ni Siku Kubwa

Wedding,Ordinary Time,Ordinary Time,WeddingEntrance
Verse 1

Ni siku kubwa njooni nyote tushangilieni

Kweli kwa shangwe na tupigeni vigelegele

Twaomba Mungu Baba Awabariki awajalie na watoto

Verse 2

Ni siku kuu ya harusi siku ya furaha

Kwani wawili wamepatana kufunga ndoa

Lindeni ndoa yenu Ili kwa dhiki wala faraja msitengane

Verse 3

Mungu alipomuumba mwanamume Adamu

Akamuumbia mwanamke waishi pamoja

Agano lake Mungu Msilivumje, msilitupe, mhifadhi.

Verse 4

Basi wewe mwanamume umpende mke wako

Umlinde na kumtunza asiwe na upweke

Umlinde siku zote Hadi mwenyezi Mungu atakapoamua

Verse 5

Na wewe mwanamke umpende mume wako tu

Na watoto mtakaojaliwa naye Mungu

Uwatunze kwa wema, na kanisani uwapeleke kwake Mungu