Ni Neema

Wedding,Ordinary TimeThanksgiving
Verse 1

Tunafanya kazi kwa juhudi na nguvu nyingi tena tunajituma

Mafanikio yake tunayaona wazi kwa macho yetu

Tunaridhika na kujiona tunafanya sisi

Kwa nguvu na akili zetu tunasahau ya kwamba hizi ni neema

Chorus

{ Ni neema (neema) mi neema (ni neema)

Ni neema (neema) zake mwenyezi } *2 Mungu

Verse 3

Na elimu tunapata kwa gharama kubwa tena elimu ya juu

Na tunadhani kwamba ni akili zetu za kibinadamu

Tunagundua vitu vipya bora na vya kisasa

Vya kuvutia eti tekinolojia yetu imekua wapendwa

Verse 4

Turudishe sifa utukufu na enzi kwa Mungu aliyetuumba

Na tuwe na hofu kwake kwani yeye anatupa yote

Tunayaweza yote katika yeye peke yake,

Tunayaweza haya yote ni kwa yeye atutiaye nguvu kweli

Verse 5

{ Piga vigelegele*3

Piga makofi piga vigelegele piga makofi }

Yeye ndiye nguvu yetu, Yeye ndiye ngao yetu

Yeye ndiye shibe yetu yeye ndiye Mungu wetu milelen{Piga makofi} *6

Piga vigelegele *3

Piga makofi *3