SectionsEntranceNi Kweli Amezaliwa

Ni Kweli Amezaliwa

Christmas,ChristmasEntrance
Chorus

Ni kweli amezaliwa Mkombozi wetu Masiha

Malaika wanaimba kwa furaha wakimsifu Bwanan{Na sisi tunafurahia Mkombozi wetu kazaliwa

Na utumwa umetutoka aleluya tushangilie } *2

Verse 2

Kwenye mji wa Daudi Mkombozi kazaliwa

Wote twende tukamwone amelazwa manyasini

Verse 3

Tuna haki kufurahi tumepata Mkombozi

Amekuja tukomboa hivyo wote tufurahi

Verse 4

Utukufu juu Mbinguni, na amani duniani

Kwa watu wote wenye mapenzi mema aleluya

Verse 5

Bwana Yesu kazaliwa, amekuja tukomboa

Katuletea wokovu, hivyo tuimbe aleluya