SectionsThanksgivingNashukuru Baba

Nashukuru Baba

Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary TimeThanksgiving
Verse 1

Nakushukuru Baba (shukuru), Baba Mwenyezi Mungu

Mwenyezi kwa kuwa umeniumba

Nakushukuru Baba (shukuru), Baba Mwenyezi Mungu

Mwenyezi kwa kuwa umeniumba

Chorus

Nitakulipa nini ee Mungu, wangu cha kukupendeza wewe

Baba mimi sina kitu chochote

Cha kulinganisha na ukarimu wako

Maombi yangu uyapokee, na dua zangu zikufikie

Kwa huruma yako Baba nisamehe

Mimi kwa makosa niliyoyatenda

Tafadhali Baba uniongezee siku nyingi ili nikutumikie

Verse 3

Nakutukuza Baba (tukuza), wewe ni ngome yangu

Ngome yangu ndiwe unayenilinda

Pokea sifa Baba (pokea) sifa ni zako wewe,nzako wewe Baba Mwenyezi Mungu

Verse 4

Nakuabudu Baba (abudu), Baba Mlinzi wangu -

Mlinzi kwa kuwa wewe ni mwema

Uniongoze Baba (ongoze), katika kweli yako,

Kweli yako nifanye mapenzi yako

Verse 5

Bwana nifanye mimi (nifanye), chombo cha kazi yakonkazi yako nikutumikie wewe

Pasipo na amani (pasipo), pasipo na upendo,nupendo nitangaze Jina lako

Verse 6

Usiniache Baba (ee Baba), uwe nami daima

Daima katika maisha yangu,

Nikufuate wewe (fuate), daima siku zote,nsiku zote milele hata milele