Chorus
Napiga goti langu (Bwana), nainamisha kichwa (chini)n{Kukuomba ewe Mungu-, unifungue moyo-
Nipate kushiriki- karamu takatifu-
Ili roho yangu dhaifu ipate wokovu} * 2
Verse 2
Furaha ya moyo wangu ni wewe Bwana
Matumaini ya moyo wangu ni kwako
Ninajongea sasa kushiriki karamu takatifu, Bwana, wangu
Verse 3
Ninaitikia mwaliko wako Bwana
Moyo wangu unatetemeka kwa hofu
Mwaliko wako umejaa upendo kwangu moyoni
Verse 4
Kila tuulapo mwili wa Bwana Yesu
Na kuinywa damu tunapata uzima
Tumekombolewa kwa damu yake Mwanakondoo, Mwana wake Mungu