Verse 1
Kwa ujasiri kwa sauti kubwa,nnazitangaza sifa za mama [Maria]
Nawauliza wakubwa wadogo,
Ni nani kama mama [Maria]
Chorus
Alimzaaa Mungu mwenyewe [kweli]namewakomboa wana wa Eva [wote]
Mama Maria anatuombea kwenye safarintufike salama [Mama Maria]
Atungojea kule kwa mwanayenatupokee tuishi salama *2
Verse 3
Kwa sifo tele kwa shangwe nderemo,
Tujitokeze mbele za mama [Maria]
Tucheze ngoma tupige makofi,nvigelegele heko kwa mama [Maria]
Verse 4
Salamu Mama umebarikiwa,
Na baraka kuliko wote [Maria]
Mzao wako amebarikiwa,
Yesu mwanao ni Mungu kweli [Maria]
Verse 5
Tukimbilie ulinzi wa mama,
Tufunuliwe siri za Mbingu[Maria]
Tupate shibe tupate neema,
Tuwe na heri hata milele [Maria]