SectionsEucharistNakula Mwili Wa Yesu

Nakula Mwili Wa Yesu

Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary TimeEucharist
Verse 1

Nakula mwili wa Yesu, nakunywa damu ya Yesu

Naburudika daima, narukaruka na Yesu

Naimba wimbo wa Yesu, nachezacheza na Yesu

Natembea naye Yesu, naenda kwetu Mbinguni

Chorus

{ Mimi nashangalia, (mimi) mimi naburudika

Yesu ameniponya, kweli nina uzima } *2

Verse 3

Mwalimu wangu ni Yesu, tabibu wangu ni Yesu

Mlinzi wangu ni Yesu, mimi nina usalama

Uhai wangu ni Yesu, mapito yangu ni Yesu,

Naenda na Bwana Yesu, naelekea Mbinguni

Verse 4

Rafiki wangu ni Yesu, jabali wangu ni Yesu

Mshindi wangu ni Yesu, mimi nitashinda vita.

Mpaji wangu ni Yesu , mlishi wangu ni Yesu

Mjali wangu ni Yesu, sina budi kumsifu

Verse 5

Kaeni ndani ya Yesu, kaeni pamoja naye

Na Yesu akae kwenu, mtashinda majaribu

Shikeni maneno yake, jifunzeni kwake Yesu

Yesu atawachukua, awapeleke Mbinguni

Verse 6

Maisha ya duniani, pasipo Yesu ni bure

Uzima wa ulimwengu, bila Yesu ni hapana

Kuleni mwili wa Yesu, kunyweni damu ya Yesu

Onjeni damu ya Mbingu, mtaishi siku zote