Nakuja Kwako Mbiombio
Nakuja kwako mbiombionnakuja kwako Mungu wangu.
Nilicho nacho mikononinninakileta mbele zako.n(Pokea Baba sehemu ya mapato niliojaliwa.
Nakutolea ingawa ni kidogo sana kibariki.
Unipe nguvu na hekimanniwe salama siku zote) x2n
Nimekuja kwa shangwe kubwannimejaa furaha tele.
Kwa vigelegele na nyimbonninaleta sadaka yangu.
Nacheza cheza bila hayanbila hofu mbele zake.
Niliokabidhiwa bureninanipasa kweli nitoe bure.
Nimepata furushi langunkisha nitoe shukrani zangu.
Bila wivu bila uchoyo ninakuja kukushukuru.
Nakuja bila dukuduku ninakuja kwa upendo.
Nakuja kusema asante
Mungu Baba kwa mema niliyopata.
Fedha zetu za mifukoninninaleta kama sadaka.
Mifugo ninao wafuganninaleta kama zawadi.
Mavuno yote ya shambaninninaleta mbele zako,
Ni matunda ya jasho langunninakupa kwa moyo wa ukarimu.
Upokee mkate huunkutoka kwa zao la ngano.
Pokea na divai hii toka tunda la mzabibu
Geuza mwili wake Yesunchakula cha waumini,
Geuza damu yake Yesunkinywaji chetu sisi tuaminio.
Moyo wangu uhai wangunmwili wangu ni mali yako.
Nguvu zangu maisha yangunninaleta ni mali yako
Nakuja na unyenyekevunninaomba shime yako,
Naomba unipe fadhila,nrehema na baraka za siku zote