Verse 1
[ t ] Naja kwako Bwana na fedha zangu chache,n[ t/b ] Japo ni kidogo naomba upokee
Chorus
Naja, kwako Bwana, naja, kwako Bwana,
Naja kwako Bwana na changu mkononi
Verse 3
Nashika mkate pia nayo divai,
Zao ya mashamba ee Bwana ninaleta
Verse 4
Umenipa vingi ee Bwana nashukuru
Nami narudisha ijapo ni kidogo
Verse 5
Natambua Bwana wewe uliniumba
Nami nashukuru wewe uliniumba