SectionsExitNaitazama Imani Yangu

Naitazama Imani Yangu

Lent,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Christmas,Easter,Ordinary Time,Ordinary Time,Lent,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary TimeExit
Verse 1

Natazama upande upande nikisema haya,

Siyo kwamba mimi naogopa maadui zangu

Nataka wote wayasikie wamwamini Mungu

Chorus

{ Naitazama imani yangu isiyumbeyumbe (kabisa) Nayatazama matendo yangu yasirudi nyuma (ah)

Upendo wako ni raha yangu ndani ya roho

Kikombe kile chake shetani mimi nisikinywe

Kabisa aaa ah kabisa 1(ni mimi ninasema) } *2

Verse 3

Umenitoa mbali ee Mungu siwezi kusema,

Wengi waliniita mgumba sasa nanyonyesha

Nataka wote wayasikie wamwamini Mungu

Verse 4

Waliponidharau mnyonge mimi sina mali,

Leo umenibariki mimi ninaishi vema,

Nataka wote wayasikie wamwamini Mungu

Verse 5

Kazi zangu nilizozifanya walizidharau

Kupitia kwa mkono wako umeniinua

Nataka wote wayasikie wamwamini Mungu

Verse 6

Shukurani yangu ninatoa kwako Mungu wangu

Sina cha kulipa mema mengi ulotenda kwangu

Nataka wote wayasikie wamwamini Mungu