Verse 1
Nainua moyo wangu kwako wewe ee Baba,
Unikinge na uovu, tumaini wewe tu
Verse 2
Nijulishe njia zako nifundishe ukweli
Hekimayo niongoze, tumaini wewe tu
Verse 3
Ee Baba ukumbuke wema wako milele,
Nifutie dhambi zangu, tumaini wewe tu
Verse 4
Nitazame kwa huruma ewe Mungu amini,
Nitubishe mwenye dhambi, tumaini wewe tu
Verse 5
Shida zangu angalia, niokoe dhikini
Nisamehe dhambi zangu, tumaini wewe tu
Verse 6
Njia zako zote Bwana nifadhili na kweli
Niongoze mtoto wako, tumaini wewe tu