SectionsEucharistMwokozi Wangu Yesu

Mwokozi Wangu Yesu

Lent,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Christmas,Easter,Ordinary Time,Ordinary TimeEucharist
Chorus

Mwokozi wangu Yesu hakika unanipenda

Umenilisha mwili na damu umeninyweshan(Yesu) Yesu asante sana sana nakushukuru

Yesu asante sana sana nakushukuru

Verse 2

Bwana wangu Yesu hakika ninakupenda sana

Moyo wangu mimi ninakutolea wewe Yesu

Umenikaribisha mimi katika karamu hiyo

Karamu ya chakula kilichoshuka toka mbinguni

Verse 3

Mwili wake Yesu chakula cha roho zetu sisi

Damu yake Yesu kinywaji cha roho zetu sisi

Wana heri wale wote wanaokula mwili wake

Na kuinywa damu yake maana wataishi na Yesu

Verse 4

Umenipa mwili na damu yako umeninywesha

Umenishibisha na pia umeniburudisha

Umeniimarisha najua sitapata njaa

Hata kiu sitapata nikiwa na wewe Yesu wangu

Verse 5

Mwamba wangu mimi ni wewe Yesu Mwokozi wangu

Nguvu zangu mimi ni wewe Yesu Mwokozi wangu

Nakutegemea Yesu najua sitaaibika

Na matumaini yangu nifike mbinguni kwako wewe