Chorus
Mwimbieni,
Mwimbieni Bwana, mwimbieni Bwana,
Mwimbieni, mwimbieni Bwana wimbo mpya,
Kwa maana,
Ametenda Bwana, mambo ya ajabu,
Kwa maana Bwana ametenda maajabu,nn{ Inueni sauti zenu, imbeni kwa furaha
Imbeni na zaburi mshangilieni Mwokozi } *2
Verse 2
Mkono wa kuume, mkono wake mwenyewe
Mkono wake wa kuume umetenda wokovu
Verse 3
Ameufunua, Bwana amefunua
Wokovu wake machoni kwa mataifa yote
Verse 4
Miisho yote, miisho ya dunia
Imeuona wokovu, wokovu wake Bwana