SectionsEntranceMwimbieni Bwana Zaburi

Mwimbieni Bwana Zaburi

Lent,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary TimeEntrance
Chorus

Mwimbieni Bwana zaburi

Mwimbieni kwa kinubi) *2n{Mwimbieni kwa kinubi na sauti ya zaburi

Mwimbieni kwa panda na sauti ya baragumu (wote)

Shangilieni mbele za mfalme Bwana wa majeshi}

Verse 2

Bahari na ivume na vyote viijazavyo,

Ulimwengu na wote wanaokaa ndani yake

Milima naiimbe kwa furaha mbele za Bwana Mungu

Verse 3

Wanyama wa mwituni na mimea ya kondeni

Upepo na uvume kupeleka habari hizi

Kwa ndege wa angani na viumbe vilivyo baharini

Verse 4

Nikitazama kushoto kulia nyuma na mbele

Nikitazama angani nikitazama ardhini

Kila nionacho kinasimulia utukufu wako

Verse 5

Kwa maana mbingu na dunia ni kazi yako

Jua na mwezi na nyota anga pia nayo mawingu

Ni kazi ya vidole vyako na ujuzi wa mikono yako