SectionsExitMwavuli Wangu

Mwavuli Wangu

Ordinary TimeExit
Chorus

Mimi niliutafuta mwavuli wangu uko wapi, wapi?

Ili niufungue, niishi chini ya mwavuli

Nisinyeshewe na yasiyopendeza Mungu (wangu)

Nisichomwe na yasiyopendeza Mungu (wangu)

Nayo yote yale yasiyo matakatifu, (Mwavuli)

Niliupata mwavuli wangu ni Yesu (Kristu)

Wa kila siku mwavuli wangu ni Yesu (Kristu)

Mchana pia usiku popote anilinda, (Ni Yesu)

Verse 2

Ananilinda na maadui, ananilinda na maadui

Na wasiopeenda amani, ananilinda na maadui

Kuliko majibu yote mi, kuliko majibu yote mi,

Niepuke mitego, ya muovu

Verse 3

Mwili wake na damu yake, mwili wake na damu yake

Matendo ya haki na ukweli *2

Dua yangu na maombi yangu, dua yangu na maombi

Mwavuli wangu mimi, damu yake