SectionsExitMwasumbukia Mambo Gani

Mwasumbukia Mambo Gani

Ordinary TimeExit
Verse 1

Enyi wanadamu mwasumbukia mambo gani

Ya Mungu ya Mungu, ya shetani ni ya shetani

Msijisumbue mle nini mvae nini

Kwani Baba yenu wa Mbinguni amewapangia

Chorus

Tazameni hawa ndege wa angani,

Hawalimi hawavuni, wanaishi,

Ninyi si zaidi ya ndege hawa

Mna haki ya kubarikiwa na Baba yangu *2

Verse 3

Mnahangaika kufanya kazi kila siku

Na mnazeeka hata bila ya kufanikiwa

Muiteni Mungu kazini hata manyumbani

Atawabariki maisha yenu yawe salama

Verse 4

Kutwa hata kucha maisha yanawasumbua

Na vijana wenu wamegeuka hohe hahe

Heshima hakuna mmebaki mkiwalilia

Mkabidhi Mungu matatizo ya familia

Verse 5

Maisha mazuri mnakula mkibakisha

Lakini kwa ndani mawazo yanawamaliza

Usoni ni raha lakini ndani mwaumia

Mkabidhi Mungu matatizo ya kibinafsi

Verse 6

Mchana wa jua hata usiku wa mbalamwezi

Siyo tofauti kwake yeye asiye na raha

Kukikucha kesho asema afadhali ni jana

Hata kesho kutwa aseme afadhali ni leo

Verse 7

Yote hayo tisa, la kumi Mungu ndiye dawa

Maisha ya raha bila Mungu yote balaa

Tutubu tuombe raha ije ndani na nje

Tutabarikiwa pia tutamaliza vizuri