Verse 1
Mwana wa Mungu, Yesu Kristu,
Bwana ninakuomba unisikie.
Mimi mdhambi ninatubu.
Bwana unisafishe na damu yako. *2
Chorus
{ Bwana unisafishe, hakika sina weman(sina wema) bila neema yako,
Mimi mwenyewe sina uwezo } *2
Verse 3
Nina imani kwako Bwana,nvile ulinifia msalabani.
Ulichukua dhambi zangu,
Ukanifungulia kwako mbinguni *2
Verse 4
Mungu wa amani na mapendo,
Mimi nitatukuza jina lako kuu
Unishike mkononi,nkazi yake shetani kutupoteza *2
Verse 5
Na kazi yangu ikiisha, Bwana,
Ninatamani kuja kwako juu,
Niwe pamoja na wateule,
Tukitumikia mpaka milele. *2